Habari za Pasi


 

Mahitaji ya muombaji wa Pasi

Kwa watanzania, Ubalozi utashughulikia kupatikana kwa Pasi mpya iwapo muhusika amekalisha yafuatayo:

1. Pasi mpya

Muombaji wa Pasi atahitajika kuja na barua ya mambo ya Pasi ambayo itaambatana fomu ya maombi, inapatikana hapa (Download)

  • Cheti cha kuzaliwa cha muombaji, au hati ya kiapo inayothibitisha tarehe ya kuzaliwa, au hati ya uraia kwa muombaji (iwapo muombaji ni aria ya kuandikishwa)
  • Cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo, au hati ya uraia wa mzazi/wazazi wa muombaji
  • Angalizo: Hati ya kiapo kwa ajili ya uthibitisho wa kuzaliwa muombaji - inabidi iwe na maelezo au kiapo cha:
  • Mzazi au mlezi halali au;
  • Mtu ambaye alikuwepo mahali ambapo muombaji alizaliwa na asiwe chini ya miaka mitano (5) ya muombaji, au;
  • Ndugu wa karibu wa muombaji ambaye alielezwa habari za kuzaliwa kwa muombaji na wazazi husika.
  • Picha tano (5) za hivi karibuni, zenye rangi ya bluu ( background blue colour);
  • Pasi iliyoisha muda pamoja na kivuli chake. Ukurasa wa kwanza na ukurasa ulio na taarifa zote muhimu za muombaji

2. Hati ya Dharura

Hati ya dharura ambayo inapatikana hapa (Download), itatolewa na Ubalozi iwapo muombaji atakuwa amepatwa na matatizo mbali mbali moja wapo ni ama kupotea au kuibiwa, hivyo muombaji atatikiwa:

> kuleta maombi yake, yeye binafsi yakiwa yameambatana na barua yenye maelezo ya mazingira halisi    ya upotevu au wizi wa Pasi.

> tangazo la gazeti juu ya upotevu/wizi wa pasi.

> picha za muombaji